MKOPO WA NIWEZESHE
Mkopo huu unalenga kumsaidia Mwanachama mkopaji anapokuwa anataka kuboresha biashara yake. Kiwango cha mkopo huu ni kuanzia 100,000/= mpaka 100,000,000/= maelezo ya uhitaji wake ni kama ifuatavyo:
- 1. Mkopaji atajaza fomu maalumu ya kuomba mkopo
- 2. Mkopo huu utatolewa kwa kila mwanachama wakati wowote, kulingana na mafungu yake.
- 3. Mkopo wa niwezeshe utakopeshwa kwa mwanachama ambaye tayari ana biashara na anataka kuboresha biashara yake.
- 4. Kabla chama hakijatoa mkopo wa niwezeshe afisa mikopo au kamati ya mikopo itafika ili kuona na kukagua biashara ili kujiridhisha na uwezo wa biashara inayoombewa mkopo huo
- 5. Dhamana za mkopo wa niwezeshe zitakuwa ni pamoja na:-
- a. Hisa, Akiba, Amana ya mwanachama
- b. Hati mbalimbali za mali zisizohamishika
- 6. Riba yake itakuwa asilimia 2% kwa mwezi
- 7. Mkopo huu utakopeshwa kwa muda mwezi 1 hadi 2
- 8. Kiwango cha mkopo huu kitakuwa mara moja, mbili au tatu ya akiba za mwanachama
- 9. Kiwango cha mkopo kitatakiwa kuwiana na viwango maalumu vya hisa vilivyowekwa na chama.
- 10. Marejesho yatafanyika kwa mkupuo kwa kadri mwombaji alivyoomba
- 11. Mkopaji atajaza mkataba wa mkopo