MKOPO WA DHARURA
Mkopo huu unalenga kumsaidia mwanachama mkopaji anapokuwa amepata dharura ya kibiashara yake, mkopo wa dharura umegawanyika katika sehemu mbili
- 1. DHARULA INAYOHUSU MAJANGA MBALIMBALI;
- (i)Mwanachama anapokuwa amepata matatizo na anahitaji msaada haraka, mfano kifo, ajali na majanga mengine yatakayodhibitishwa na kamati ya mikopo, mkopo huu hautazidi shilingi 5,000,000/=na utarejeshwa kwa mwezi mmoja hadi minne. (ii)Riba ya mkopo huu ni 1%
- 2. DHARULA INAYOHUSISHA BIASHARA
- Mwanachama anapokuwa amepata dharura ya kibiashara mfano, fedha ya kukombolea mzigo na kuboresha biashara yake. Mkopo huu maelezo ya uhitaji wake yatadhibitishwa na kamati ya mikopo.Masharti yake ni pamoja na ;
- a. Mwombaji atajaza fomu maalum ya mkopo wa dharula
- b. Marejesho ya mkopo huu ni mwezi mmoja au miwili
- c. Riba ya mkopo huu ni 2% kwa mwezi.
- d. Kiwango cha juu cha mkopo huu kitakuwa shilingi 200,000,000/= na itategemea dhamana pamoja na biashara ya mwombaji.
- e. Mwanachama ataruhusiwa kukopa mkopo huu endapo amerejesha nusu ya mkopo wake wa biashara.(vinginevyo kuwe na nyaraka maalum zinazoonyesha umuhimu wa kupewa mkopo huu)
- f. Mkopo huu hautatolewa kwa kujirudiarudia kila mwezi isipokuwa kama kuna sababu maalumu.
- g. Mkopaji atajaza mkataba wa mkopo.
- h. Mwanachama atapata mkopo huu bila kuweka mafungu ya Hisa na Akiba kwani mkopo huu ni huduma kwa Wanachama.