Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
MKOPO MAALUM WA BIASHARA (COMMERCIAL SPECIAL LOAN)

Mkopo huu unalenga kumsaidia Mwanachama au asasi zingine za kifedha kuendesha shughuli zake za biashara kwa kumuongezea mtaji na hivyo kuleta kasi ya mzunguko wa biashara yake na kukabiliana na ushindani wa biashara kwa riba nafuu.

Mkopo huu una masharti yanayofanana na mkopo wa biashara lakini wenyewe kiwango chake ni kuanzia milioni mia tatu (300,000,000/=) na kiwango cha juu ni milioni mia sita (600,000,000/=)

Mkopo maalum utakopeshwa kwa mwanachama ambaye tayari ana biashara inayowiana na kiasi cha mkopo kinachoombwa.

  • Mkopaji atajaza fomu maalumu ya mkopo
  • Kabla chama hakijatoa mkopo maalumu afisa mikopo, meneja au kamati ya mikopo itafika ili kuona na kukagua biashara ili kujiridhisha na uwezo wa biashara inayoombewa mkopo huo.
  • Dhamana za mkopo maalumu zitakuwa ni pamoja na
  • a. Hisa, Akiba, Amana ya mwanachama
  • b. Hati mbalimbali za mali zisizohamishika
  • Riba yake itakuwa asilimia 1.5%
  • Mkopo huu utakopeshwa kwa muda wa miezi sita hadi Arobaini na nane (48)
  • Kiwango cha mkopo huu kitakuwa mara moja, mbili au tatu ya akiba za Mwanachama
  • Kiwango cha mkopo kitatakiwa kuwiana na viwango maalumu ya hisa vilivyowekwa na chama.
  • Mwanachama hataruhusiwa kuwa na mkopo wa biashara pamoja na mkopo maalum wa biashara kwa wakati mmoja.
  • Mwanachama hataruhusiwa kukopa mkopo maalum endapo hajarejesha mkopo wa dharura
  • Mwanachama anayeruhusiwa kukopa mkopo huu ni yule aliyejiunga zaidi ya mwaka mmoja ndani ya ushirika wa LULU SACCOS
  • Mwombaji atakayekuwa na sifa za kupata mkopo huu atapewa mkataba na kuujaza.
  • Maombi yote ya Mkopo maalum yatajadiliwa na Kamati ya Mikopo, na kuidhinishwa na Bodi ya LULU SACCOS.
  • News 1
    Karibu Sana

    Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

    picture-ya-Pesa
    Vyanzo vya Mapato

    • (a) Hisa za wanachama
    • (b) Malimbikizo ya faida
    • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
    • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
    • (e) Akiba za wanachama
    • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

    Ufahamu Zaidi

    BIMA YA MIKOPO

    Brief description of the news or event.

    Read More
    USIMAMISHAJI MIKOPO

    Brief description of the news or event.

    Read More
    UREJESHAJI WA MIKOPO

    Brief description of the news or event.

    Read More