Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
MKOPO WA MAENDELEO (NYUMBA, VIWANJA NA VIFAA VYA UJENZI)

Mkopo huu unalenga kumuwezesha mkopaji kufanya Maendeleo binafsi kwa kununua Nyumba/Viwanja. Mahitaji ya mkopo huu ni pamoja na haya yafuatayo:-

  • 1. Mkopaji atajaza fomu maalum ya kuomba mkopo huu.
  • 2. Mkopaji ana hiari ya kuchagua muda wa marejesho kuanzia miezi mitatu (3) hadi miezi ishirini na nne (24).
  • 3. Riba ya Mkopo wa Maendeleo ni Asilimia mbili 1.5%.
  • 4. Mkopaji anaweza kukopa mkopo ambao ni mara moja(1) Mbili (2) au tatu (3) ya Akiba alizojiwekea
  • 5. Mkopaji atahitajika kuwa na kiasi cha Hisa zinazowiana na viwango vilivyowekwa kwa viwango mbalimbali vya mikopo
  • 6. Mkopaji atatafuta mwenyewe uwanja au nyumba inayokusudiwa kununuliwa.
  • 7. Nyumba au kiwanja ni lazima kiwe na Nyaraka za kuonyesha uhalali wa umiliki wa muuzaji.
  • 8. Afisa Mikopo na Kamati ya Mikopo watafuatilia umiliki wa Mali hiyo ili kuthibitisha uhalali wake na kujiridhisha kuwa mali hiyo haijatumika kuchukulia mkopo mahali pengine.
  • 9. Nyaraka za Mali hiyo zitabaki kwenye Ofisi za LULU baada ya kununulia kwa kutumia fedha za Mkopo hadi pale Mkopaji atakapo kamilisha malipo ya mkopo wake.
  • 10. Dhamana ya mkopo huu ni pamoja na:- Hisa, Akiba, Amana ya mwanachama - (i) Mradi wenyewe kupitia biashara akaunti (ii) Hati mbalimbali za mali ya umiliki
  • 11. Kiwango cha juu cha mkopo huu kitakuwa ni Tshs.100, 000,000/=
  • 12. Dhamana itakuwa ndani ya Mkoa wa Mbeya.
  • 13. Mwanachama anayeruhusiwa kukopa mkopo huu ni yule aliyejiunga zaidi ya mwaka mmoja ndani ya Ushirika huu.
  • 14. Kwa mkopo wa vifaa vya ujenzi, mkopaji atatoa mchanganuo wa vifaa vinavyohitajika na jumla ya bei kwa vifaa vyote.LULU SACCOS itampa fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya ujenzi.
  • 15. Mkopaji atapaswa kujaza mkataba wa mkopo.
News 1
Karibu Sana

Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

picture-ya-Pesa
Vyanzo vya Mapato

  • (a) Hisa za wanachama
  • (b) Malimbikizo ya faida
  • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
  • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
  • (e) Akiba za wanachama
  • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

Ufahamu Zaidi

BIMA YA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
USIMAMISHAJI MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
UREJESHAJI WA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More